Hungaria
| |||||
| Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
| Wimbo wa taifa: Himnusz ("Isten, áldd meg a magyart") "Wimbo" ("Mungu wabariki Wahungaria wote") | |||||
| Mji mkuu | Budapest | ||||
| Mji mkubwa nchini | Budapest | ||||
| Lugha rasmi | Kihungaria (Magyar) | ||||
| Serikali | Serikali ya kibunge Jamhuri Tamás Sulyok Viktor Orbán | ||||
| Uhuru Principality of Hungary Ufalme wa Hungaria Kuachana kwa Milki ya Austria-Hungaria Jamhuri ya Hungaria |
896 Desemba 1000 1918 1989 | ||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
93,030 km² (ya 109) 0.74% | ||||
| Idadi ya watu - 2024 kadirio - 2023 sensa - Msongamano wa watu |
9,580,000 (ya 95) 9,599,744 103/km² (ya 78) | ||||
| Fedha | Forint ya Hungaria (HUF) | ||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
| Intaneti TLD | .hu 1 | ||||
| Kodi ya simu | +36 | ||||
| 1 pia .eu kama nchi ya Umoja wa Ulaya | |||||
Hungaria (kwa Kihungaria Magyarország), rasmi kama Jamhuri ya Hungaria, ni nchi isiyo na pwani katika Ulaya ya Kati, inayopakana na Slovakia kaskazini, Ukraini kaskazini-mashariki, Romania mashariki, Serbia na Kroatia kusini, Slovenia kusini-magharibi, na Austria magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 9.6, ikiwa ya 94 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Budapest. Hungaria imegawanyika katika mikoa 19 na jiji la Budapest.
Kihungaria ndiyo lugha rasmi na ya kawaida kwa wananchi.
Wakazi walio wengi (52.9%) ni Wakristo. hasa Wakatoliki (37.4%) na Wakalvini (11.1%).
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Topografia
[hariri | hariri chanzo]
Hungaria ni nchi isiyo na pwani iliyoko Ulaya ya Kati, yenye mandhari ya mteremko laini na tambarare kwa sehemu kubwa. Nchi hii imegawanywa katika maeneo makuu mawili: tambarare za chini (Alföld au Tambarare kuu ya Hungaria) upande wa mashariki na kusini, na milima na mteremko wa juu upande wa kaskazini na magharibi. Milima ya Kaskazini ya Hungaria, ikijumuisha milima ya Mátra na Bükk, ina kilele cha juu zaidi cha Hungaria, Kékes, kilichofikia urefu wa mita 1,014. Milima na maporomoko ya Transdanubian upande wa magharibi hutoa mandhari laini, wakati Tambarare Kuu inatawaliwa na ardhi zenye rutuba kwa kilimo. Eneo la kati la Hungaria katika Bonde la Karpathian limeunda mifumo ya makazi, kilimo, na mitandao ya usafirishaji.
Hali ya Hewa
[hariri | hariri chanzo]Hungaria ina hali ya hewa ya kikanda, yenye misimu tofauti ikijumuisha majoto makali ya majira ya joto na baridi kali za majira ya baridi. Joto la wastani la majira ya joto ni kati ya 25°C hadi 30°C , wakati joto la majira ya baridi mara nyingi hupungua chini ya 0°C , hasa katika milima ya kaskazini. Mvua hujumlisha wastani wa milimita 500–800 kwa mwaka, huku mvua ikipunguka katika milima ya kaskazini na kupungua katika tambarare. Theluji ni ya kawaida majira ya baridi, na radi zinaweza kutokea katika miezi ya majira ya joto. Mabadiliko ya msimu na mvua ya wastani husaidia kilimo, misitu, na mifumo ya maji safi.
Mfumo wa Maji
[hariri | hariri chanzo]
Hungaria ina mtandao mzuri wa mito na maziwa, sehemu kubwa zikielekea kwenye mito ya Danube au Tisza. Mto Danube, mto mrefu wa pili Ulaya, unapita kutoka kaskazini hadi kusini kupitia magharibi mwa Hungaria, ikiwemo mji mkuu Budapest, na unatumika kama njia kuu ya usafirishaji na uchumi. Mto Tisza unapita sehemu ya mashariki ya nchi, huku mito midogo, vyanzo, na mifereji ikisaidia umwagiliaji na mifumo ya mazingira. Hungaria pia ina maziwa makubwa, kubwa zaidi ikiwa ni Ziwa Balaton, mara nyingi huitwa Bahari ya Hungary, ambalo ni eneo muhimu kwa utalii, uvuvi, na burudani.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]Hungaria ilitokea kama nchi ya pekee wakati wa karne ya 10 BK.
Tangu zamani za kuzaliwa kwake Kristo (milenia ya kwanza) sehemu kubwa ya Hungaria ilijulikana kama Panonia ikawa sehemu ya Dola la Roma.
Tangu kuporomoka kwa nguvu ya Waroma ilivamiwa na makabila mbalimbali kama vile Wagermanik, Wahunni na Waslavi.
Baada ya mwaka 900 Wahungaria chini ya mtemi Arpad walivamia eneo hili. Wakati ule Wahungaria walikuwa mkusanyiko wa makabila wahamiaji waliojiita "Majari" (Magyar) waliotoka katika maeneo kati ya mto Volga na milima ya Ural.
Kutoka makazi yao mapya katika Panonia waliendelea kuvamia maeneo mengine ya Ulaya hadi milima ya Pirenei.
Baada ya kupokea Ukristo
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kushindwa na Wajerumani mwaka 955 walibaki katika makazi yao na mnamo mwaka 1000 mfalme Ishtvan (Stefano wa Hungaria) alipokea ubatizo akaongoza taifa lake kuingia katika Ukristo.
Wakati wa uvamizi wa Wamongolia baada ya Chingis Khan katika karne ya 13 nchi iliangamizwa, na nusu ya wakazi wakauawa.
Baadaye wafalme Wahungaria waliwakaribisha walowezi kutoka Ujerumani walioanzisha vijiji vingi na pia miji.
Wakati wa karne ya 15 Waturuki Waosmani walianza kuenea kwenye Balkani, wakaingia katika Hungaria kutoka upande wa mashariki. Katika mapigano ya Mohacs mwaka 1526 Hungaria ilishindwa na sehemu kubwa ikawa chini ya Waosmani. Magharibi ya nchi ikaendelea kuitwa ufalme wa Hungaria lakini ufalme uliingia mikononi mwa nyumba ya Habsburg yaani chini ya watawala wa Austria.
Katika karne zilizofuata watawala wa Habsburg walirudisha Waosmani nyuma na ufalme wa Hungaria ukawa sehemu ya milki ya Habsburg yaani Austria.
Katika karne ya 19 mnamo 1848 Wahungaria waliasi dhidi ya watawala lakini walishindwa. Hata hivyo Kaisari Franz Joseph I alibadilisha siasa yake akatafuta usaidizi wa Wahungaria katika utawala wa ufalme. Katiba mpya iliunda cheo cha sawa kati ya Austria na Hungaria chini ya mtawala yeye yule mwenye vyeo vya Kaisari wa Austria na Mfalme wa Hungaria na milki ikaitwa "Austria-Hungaria".
Austria-Hungaria ilikuwa milki kubwa katika Ulaya ya Kati na Mashariki kuanzia mwaka 1867 hadi 1918.
Kuanzia karne ya 20
[hariri | hariri chanzo]Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia milki ikaporomoka na Hungaria ikaendelea kama nchi ya pekee yenye katiba ya ufalme lakini bila mfalme.
Katika vita kuu ya pili ya dunia Hungaria ikaingia upande wa Ujerumani ukaendelea kuwatesa Wayahudi wake wa kushikamana na siasa ya Hitler na mwishowe ikashindwa pamoja na Ujerumani. Hungaria ikavamiwa na jeshi la Umoja wa Kisovyeti na mabwana hao wapya walihakikisha ya kwamba chama cha kikomunisti ilishika serikali. Hivyo Hungaria ikawa sehemu ya Mapatano ya Warshawa ikasimama upande wa mashariki katika kipindi cha vita baridi.
Mwaka 1956 wananchi wengi walipindua serikali ya kikomunisti na serikali mpya chini ya Imre Nagy ilianzisha demokrasia ya vyama vingi. Lakini wanajeshi wa Kisovyeti wakaingia kati wakarudisha utawala wa chama cha kikomunisti ulioendelea hadi kuporomoka kwa ukomunisti mnamo 1989.
Hungaria imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 2004.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Nchi za Umoja wa Ulaya | |
|---|---|
| Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hungaria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
